Alhamisi, 19 Machi 2015

Ijue wilaya yetu

KYELA YETU

Wilaya ya Kyela ni wilaya moja ya Mkoa wa Mbeya.

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa

wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 174,470 [1] . Makao

makuu yapo Kyela Mjini.

Marejeo

 Tanzania.go.tz/census

Kata za Wilaya ya Kyela – Mkoa

wa Mbeya - Tanzania

★Bujonde 

★Busole

 ★Ikama 

★Ikolo

★Ipande (Kyela) 

★Ipinda 

★Kajunjumele

★Katumba Songwe 

★Kyela Mjini 

★Lusungo

★Makwale

★Matema

★Mwaya

★Ngana

★Ngonga

Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Kyela??

kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni wa watu wa kyela?


KARIBU KYELA.

TAKUKURU YAWATAJA WALA RUSHWA

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na

Rushwa (Takukuru) imetangaza katika tovuti yake
majina 287 ya washtakiwa waliopatikana na hatia
katika kesi za rushwa.
Miongoni mwa majina yaliyotangazwa kupitia
tovuti yake www.pccb.go.tz wamo
wafanyabiashara, wanasiasa, waandishi wa habari,
walimu, wauguzi, polisi, mwanafunzi na watumishi
mbalimbali wa umma.
Hatua hiyo ya Takukuru ni mwanzo wa mfumo na
utaratibu mpya ulioanzishwa na taasisi hiyo wa
kuwatangaza hadharani washtakiwa wote
waliopatikana na hatia katika kesi zinazohusu
rushwa.
Ofisa Uhusiano wa taasisi hiyo, Doreen Kapwani
alisema jana katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari kuwa, utaratibu huo ambao umeanza
kutumika Machi mwaka huu ni sehemu ya
utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa
(BRN).
Alisema utaratibu huo utasaidia kuwahabarisha
wananchi kuhusu hatua zinazochukuliwa na
Serikali katika kuwashughulikia wala rushwa.
“Kutokana na utaratibu huo, majina, taarifa
binafsi, maelezo ya mashtaka ya watu
waliopatikana na hatia, yatakuwa yanapatikana
katika tovuti ya taasisi katika sehemu yenye kichwa
cha habari ‘Wahalifu wa Makosa ya Rushwa’,”
alisema Kapwani.
Hata hivyo, Kapwani alitoa angalizo kuwa taarifa
zinazowekwa hadharani ni zile tu za washtakiwa
ambao walifunguliwa mashtaka dhidi ya rushwa na
kesi zao kutolewa hukumu na Mahakama.
Akizungunzia kuhusiana na hatua hiyo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali
linalojihusisha na Masuala ya Kijamii (Fordia),
Buberwa Kaiza alisema hiyo ni hatua nzuri lakini
haoni kama itasaidia.
“Tanzania ilipofikia karibu kila mtu ni mla rushwa.
Mbaya zaidi kuna rushwa kubwa ambazo Takukuru
imesema haiwezi kushughulika nazo... sina imani
na hatua hiyo,” alisema Kaiza na kuongeza kuwa
wanafanya hivyo ili kujionyesha kuwa wanafanya
kazi.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema:
“Sidhani kama utaratibu huo utasaidia kwa sababu
kuna watu hata majina yao yakichapishwa
hadharani hawatajali.”
Alisema kama mtu anatoa au kupokea rushwa
tayari hana hofu yoyote, hivyo hata jina lake
likichapishwa hataona shida wala kuhofia.
“Rushwa ni suala kubwa. Jambo la muhimu ni
kuanza kulishughulikia tatizo hilo kwa upande wa
maadili. Tutafute namna na kurudisha maadili…
watu wawe na maadili. Huo ndiyo utakuwa mwanzo
mzuri wa kupambana na rushwa,” alisema.

Source.mwananchi